6 Septemba 2021 - 08:51
Walimwengu waendelea kulaani mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea, Conakry

Mataifa, asasi na jumuiya mbalimbali za kieneo na kimataifa zimelaani mapinduzi ya kijeshhi ya jana huko nchini Guinea na kutiwa mbaroni Rais Alpha Conde.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi (ECOWAS, Marekani na Ufaransa zimeungana na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kulaani vikali mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea  na kutoa wito wa kuachiliwa huru mara moja, kionghozi halali wa nchi hiyo Rais Alpha Conde.

Hatima ya Rais Alpha Conde wa Guinea aliyepinduliwa bado haijafahamiki huku hali ya wasiwasi ikiwa imetanda nchini humo baada yay kuenea taarifa za kupinduliwa Rais. Vikosi maalum vya jeshi nchini Guinea Conakry vimetangaza kuwa, vimehitimisha utawala wa Alpha Conde baada ya kumpindua Rais huyo na kwamba, hivi sasa vinamshikilia mwanasiasa huyo mkongwe.

Kanali Mamady Doumbouya, Mkuu wa vikosi maalum vya jeshi la Guinea, anayeongoza kundi lawanajeshi na maafisa wa vikosi vya usalama waliofanya mapinduzi ametangaza kuunda Kamati ya Taifa kwa ajili ya Maendeleo ya Guinea, CNRD, na kuahidi kufanyika mazungumzo yasiyobagua na yenye manufaa kwa minajili ya kuandaa katiba mpya. Awali waziri wa ulinzi alinukuliwa akisema jaribio la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa.

Jeshi ambalo limedai kuchukua madaraka nchini humo limetangaza kwamba litafanya mkutano leo Jumatatu na mawaziri na wakuu wa taasisi zilizovunjwa jana mjini Conakry.

Mapinduzi hayo yanajiri baada ya kipindi kirefu cha mvutano wa kisiasa nchini Guinea. Mgogoro huo ulichochewa mwanzo na upinzani mkali dhidi ya hatua ya Rais Conde kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka uliopita.

342/